Karibu katika Tovuti yetu ya Kamisheni ya Utumishi wa Umma Zanzibar, Katika Tovuti hii utapata habari za uhakika na zilizokamilika ambazo zitakupa muongozo mzima kuhusiana na muelekeo, malengo ya kimkakati pamoja na shughuli zote zinazofanywa na Ofisi ya Kamisheni ya Utumishi wa Umma Zanzibar.
Dira Yetu
Kuwa na chombo huru na chenye uadilifu ambacho kitaleta tija na utawala bora katika Utumishi wa Umma
Dhamira Yetu
Kuongeza ufanisi katika Utumishi wa Umma kwa kuhakikisha uzingatiaji wa Sheria, Kanuni na Miongozo ya Utumishi wa Umma
Haki na Wajibu
Kamisheni ina jukumu la kusimamia Haki za Watumishi wa Umma katika Taasisi zao
Miongozo
Tuna jukumu la kuhakikisha watumishi wote wanafuata taratibu na sheria kazini.
Ufuatiliaji
Kamisheni ina wajibu wa kufuatilia uendeshaji wa shughuli za Rasilimali Watu.