Kukabidhi miundo ya Taasisi ya SMIDA na Tume ya Utumishi wa Mahakama
Katibu wa Kamisheni ya Utumishi wa Umma Ndg. Kabingwa Mashaka Simba ameitaka Tume ya Utumishi wa Mahakama pamoja na Wakala wa Maendeleo ya Viwanda Vidogo Vidogo, Vidogo na Vya kati Zanzibar kuhakisha wana chagua viongozi wenye sifa ili kuwapanga kwa mujibu Muundo wao wa Taasisi.
Katibu Kabigwa ametoa kauli hiyo ofisini kwake Mwanakwerekwe wakati akikabidhi Miundo ya Taasisi hizo
Amesema kukabidhiwa kwa miundo ya taasisi itasaidia kutekeleza Majukumu yao ya kila siku bila ya muingiliano wa nafasi zao.

Wakitoa shukrani kwa Kamisheni ya Utumishi wa Umma, Katibu wa Tume ya Mahakama pamoja na Mkurungenzi Mkuu wa (SMDA) ndugu Salum Hassan Bakari na ndugu Soud Said Ali wamesema wataitumia Miundo hio kwa kuwapanga Watumishi katika nasafi zao ili kuondoa muingiliano wa majukumu na hatimae kupelekea kupatikana tija katika utekelezaji wa kazi zao.