Ghafla ya Kuwaaga Wastaafu wa Kamisheni ya utumishi wa Umma
Katibu wa Kamisheni ya Utumishi wa Umma ndugu Kabingwa Mashaka Simba amesema wataendeleza mambo mema na tabia njema wakiwa kazini na mahali popote kwa kushirikiana pamoja na watendaji wa Taasisi za serikali ili mafanikio yaweze kupatikana kwa kasi kubwa
Katibu Kabigwa ameyasema hayo katika hafla fupi ya kuwaaga watumishi watatu waliostaafu katika Kamisheni ya Utumishi wa Umma mwanakwerekwe
Amesema lengo la kuwafanyia sherehe hiyo ni kuwakumbuka na kuthamini mchango wao walioutoa wakati walipokuwa kazini na kuishi nao vizuri katika muda wote utendaji wao.

Hata hivyo Katibu Kubingwa amesema wataendelea kuwatumia pale ambapo watahitaji kupata ushauri na mchango wao. Amesema kuondoka kwao ni jambo la lazima kwa kila mtumishi wa umma pale muda unapoisha wa kuitumikia Serikali.
Nae Mkurugenzi wa Utawala RasilimaliWatu na Mipango bi Maryam Rished Mbarouk amesema wastaafu hao walikua wakitenda haki katika utendaji wa majukumu yao na kuwasaidia wafanyakazi wengine kwa kuwapa ushauri mzuri.
Aidha bi Mryam amewapongeza kwa kuutumia muda wao vizuri hadi kufikia kustaafu kwa salama na amani ni jambo la kujivunia na kumshukuru Mungu kwani wengine hufanya makosa hadi kufikia kufukuzwa kazi.
Wakitoa shukurani wastaafu hao wamewasisitiza watendendaji wezao kushirikiana pamoja katika kazi, kupendana na kufuata sheri zote za kazi zilizowekwa ikiwa kuwa na heshima na nidhamu pamoja na kutumia lugha nzuri.
Katika sherehe hiyo wastaafu hao walikabidhiwa zawadi mbali mbali ikiwemo cheti cha nidhamu , TV flat, Feni, jagi la umeme, na mswala. Wastaafu wenyewe ni ndugu Ramadhan Mohammed Khamis, Hassan Ameir Hafidhi na bi Fatma Mkubwa Makame.