Kamisheni ya Utumishi wa Umma - ZanzibarKamisheni ya Utumishi wa Umma - ZanzibarKamisheni ya Utumishi wa Umma - Zanzibar
+255 (24) 2230034
kamisheni.utumishi@zpsc.go.tz
Zanzibar, Tanzania
Kamisheni ya Utumishi wa Umma - ZanzibarKamisheni ya Utumishi wa Umma - ZanzibarKamisheni ya Utumishi wa Umma - Zanzibar

KAMISHENI YA UTUMISHI WA UMMA YAKABIDHI MUUNDO WA TASISI WA ZRA

Kamisheni ya Utumishi wa Umma imeikabidhi Mamlaka ya Mapato Zanzibar (ZRA) Muundo wa taasisi hiyo kufuatia mabadiliko ya kimuundo kutoka iliyokua Bodi ya Mapato Zanzibar yaliyotokea hivi Karibuni.

Akizunguza baada ya kukabidhi Muundo huo Katibu wa Kamisheni ya Utumishi wa Umma ndugu Kubingwa Mashaka Simba aliipongeza ZRA kuja na Muundo mpya unaokwenda smbamba na kasi ya serikali ya awamu ya nane (8).

Katibu Kubingwa alisema Muundo huo wnye jumla ya idara nane (8) na vitengo sita (6) pamoja na ofisi za Mikoa, unatarajiwa kupunguza gharama za uendeshaji kwa wastani wa  shilingi milioni 37 kwa mwezi ikilinganishwa na muundo wa awali.

Aidha, Katibu huyo alisema mabadiliko haya ya muundo wa ZRAyamefanyika ili pamoja na kurahisisha utekelezaji wa majukumu ya taasisi, bali pia ni kwa lengo la kuendana namiundo ya taasis nyengine za kikanda za ukusanyaji wa kodi.

 Katibu kubingwa alisisitiza kuwa baada ya makabidhiano ya muundo huo, Mamlaka ya Mapato Zanzibar inapaswa kuanza mara moja matumizi yake ili kukidhi matarajio ya Serikali katika ukusanyaji wa mapato.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa Muundo huo, Kamishna Mkuu wa mamlaka ya Mapato Zanzibar Ndg Yussuph Juma Mwenda alisema ZRA itautekeleza Muundo huo zaidi ya matarajio ya serikali na kuongeza kuwa utaongeza ufanisi katika ukusanyaji wa kodi.

 Alifafanua kuwa Muundo huo umesadifu muelekeo wa ufanyaji kazi wa Taasisi za kodi duniani na kwamba nafasi za uongozi katika Muundo huo zitajazwa kwa mfumo wa ushindani kama ilivyoelekezwa na sheria. Muundo huo mpya wa ZRA pamoja na mambo mengine unatoa nafasi kwa mabadiliko ya vyeo vya taasisi hiyo ambapo sasa Kutakua na Kamishna,Wakurugenzi, Wakuu wa Vitengo pamoja na Wakuu wa Divisheni.

Leave A Comment

Subscribe to our newsletter

Sign up to receive latest news, updates, promotions, and special offers delivered directly to your inbox.
No, thanks