Kamisheni ya Utumishi wa Umma - ZanzibarKamisheni ya Utumishi wa Umma - ZanzibarKamisheni ya Utumishi wa Umma - Zanzibar
+255 (24) 2230034
kamisheni.utumishi@zpsc.go.tz
Zanzibar, Tanzania
Kamisheni ya Utumishi wa Umma - ZanzibarKamisheni ya Utumishi wa Umma - ZanzibarKamisheni ya Utumishi wa Umma - Zanzibar

Katibu wa Kamisheni ya Utumishi wa Umma akimkabidhi Naibu Mwanasheria Mkuu w Zanzibar Muundo wa Taasisi wa Afisi ya Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar.

  • Home
  • Business & Strategy
  • Katibu wa Kamisheni ya Utumishi wa Umma akimkabidhi Naibu Mwanasheria Mkuu w Zanzibar Muundo wa Taasisi wa Afisi ya Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar.

Wilaya ya magharibi B Unguja.
Katibu wa Kamisheni ya Utumishi wa Umma ndugu Kubingwa Mashaka Simba ameitaka Taasisi ya Mwanasheria Mkuu Zanzibar kuhakisha kuwa muundo ulikabidhiwa unatekelezwa ili kukidhi mahitaji ya watumishi pamoja na wananchi wa Zanzibar kwa ujumla ndani ya Taasisi hiyo kwa kuchagua watendaji wazuri wanaoenda na sifa na ufanisi ikiwemo wenye sifa ya Elimu na kuwepo kwa uzoefu wa kazi ili kwenda sambamba na maagizo ya Serikali ya mapinduzi ya zanzibar .
Ndugu Kubingwa ametoa wito huo wakati akimkabidhi muundo ndugu Shaabani Ramadhan Abdallah ambaye ni Naibu Mwanasheria Mkuu zanzibar wa Taasisi ya Mwanasheria Mkuu hapo ofisini kwake Mwanasheria

Amesema muundo huo ni muendelezo ya majukumu yaliyoanishwa humo ambao unaogoza jinsi ya kufuata maelekezo ili kurahisisha kazi kwa watendaji wa Taasisi na kuleta faida na mafanikio yaliyo mazuri.
Aidha katibu wa kamisheni ya utumishi wa Umma ndugu Kubingwa ameishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuidhinishwa sheria hiyo ya kuwepo kwa muundo unaoongoza jinsi gani waterndaji na viongozi kufuata kanuni na sheria zilizomo ndani yake na pia amewasisitiza viongozi hao kuchagua viongozi wenye uweled ili kuepuka ubabaishaji
unaofanfwa na baadhi ya taasisi kwa kupunguza malalamiko yanayojitokezaili kila mwananchi na watendaji wapate haki zao za msingi.

Akitoa shukurani kwa niaba ya taasisi ya Mwanasheria Mkuu Naibu Mwanasheria Mkuu ndugu shaabani Ramadhan Abdallah ameipongeza taasisi ya Kamisheni ya utumishi wa Umma Zanzibar kwa kazi nzuri iliyofanywa kwa wakati muafaka ya kuaanda muundo huo na kuahidi yale yote waliyopewa watayafanyia kazi hasa wakizingatia kwamba taasisi hiyo imekuwa ikijishughulisha ma mambo mengi ikiwemo kesi za aina mbali mbali kwa wananchi na watendaji wa Taasisi za serikali
Hata hivyo wameahidi kuleta mashirikiano kati yao na taasisi nyengine ili mafanikio yaweze kupatikana kwa haraka zaidi ili keenda kasi na utendaji wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi.

Leave A Comment

Subscribe to our newsletter

Sign up to receive latest news, updates, promotions, and special offers delivered directly to your inbox.
No, thanks