Idara ya Miongozo na Uchambuzi wa Miundo
Idara hii itahusika na majukumu ya utayarishaji wa miongozo na matoleo mbali mbali yatayotolewa na Kamisheni, kutoa maoni na mapendekezo juu ya miundo ya taasisi, utumishi, mishahara, maposho na maslahi mengineyo ya taasisi mbali mbali za umma.
Majukumu
- Kupokea, kuchambua, kutoa maoni na mapendekezo ya miundo mbali mbali inayowasilishwa Kamisheni.
- Kuandaa, kuchapisha, kusambaza na kuitangaza miongozo mbali mbali inayotolewa na Kamisheni.
- Kupendekeza njia bora na mifumo ya uendelezaji na usimamizi wa Utumishi wa Umma.
- Kuandaa na kutoa matoleo mbali mbali yanayohusiana na usimamizi wa Utumishi wa Umma.
- Kutoa ushauri na mapendekezo ya uanzishwaji wa wizara na taasisi mbali mbali katika Utumishi wa Umma.
- Kufanya utafiti unaohusiana na kazi za idara ili kurahisisha utekelezaji wa majukumu ya idara.
- Kupendekeza mifumo ya usimamizi wa utumishi wa umma.
- Kuandaa Ripoti za utekelezaji wa kazi za Idara.
Idara hii ina divisheni tatu (3) ambazo ni Divisheni ya Uchambuzi wa Miundo ya Wizara Wakala Tendaji na Mashirika ya Umma na Divisheni ya Uchambuzi wa Miundo ya Tawala za Mikoa na Taasisi Zinazojitegemea, Divisheni ya Miongozo na Matoleo.
Divisheni ya Uchambuzi wa Miundo ya Wizara, Wakala Tendaji na Mashirika ya Umma.
Divisheni hii itahusika kufanya uchambuzi na kutoa maoni na mapendekezo ya miundo ya taasisi, utumishi, mishahara na maslahi mengine katika Wizara, Wakala Tendaji na Mashirika ya Umma.
Divisheni ya Uchambuzi wa Miundo ya Tawala za Mikoa na Taasisi Zinazojitegemea
Divisheni hii itahusika kufanya uchambuzi na kutoa maoni na mapendekezo ya miundo ya taasisi, utumishi, mishahara na maslahi mengine katika Taasisi zilizopo chini ya Tawala za Mikoa na Taasisi Zinazojitegemea.
Divisheni ya Miongozo na Matoleo
Divisheni hii itahusika na utayarishaji, uchapishaji, usambazaji na utangazaji wa miongozo na matoleo kupitia mbali mbali inayotolewa na Kamisheni.

Mahfoudh M. Hassan
Mkurugenzi- Idara ya Miongozo na Uchambuzi wa Miundo