Kamisheni ya Utumishi wa Umma - ZanzibarKamisheni ya Utumishi wa Umma - ZanzibarKamisheni ya Utumishi wa Umma - Zanzibar
+255 (24) 2230034
kamisheni.utumishi@zpsc.go.tz
Zanzibar, Tanzania
Kamisheni ya Utumishi wa Umma - ZanzibarKamisheni ya Utumishi wa Umma - ZanzibarKamisheni ya Utumishi wa Umma - Zanzibar

Idara ya Rasilimali Watu, Utawala na Mipango

 • Home
 • Idara ya Rasilimali Watu, Utawala na Mipango
Maelezo
Idara ya Rasilimali Watu, Utawala na Mipango

Idara hii itahusika na majukumu ya utawala, uendeshaji, usimamizi na uendelezaji wa rasilimali watu, uandaaji na ufatiliaji wa mipango ya taasisi na utunzaji wa kumbukumbu wa nyaraka mbali mbali zinazohusiana na utumishi wa umma pamoja na kusimamia shughuli za masjala.

Idara hii inapendekezwa kuwa na divisheni nne (4), ambazo ni Divisheni ya Rasilimali Watu, Divisheni ya Utawala, Divisheni ya Mipango na Takwimu na Divisheni ya Kumbukumbu. 

 Majukumu

 • Kuunganisha shughuli zote zinazofanywa na Idara za Kamisheni.
 • Kutoa huduma na matayarisho ya kuiwezesha Kamisheni kufanya kazi zake ipasavyo, ikiwemo vikao na ziara za Makamishna.
 • Kusimamia rasilimali zote za Kamisheni.
 • Kuandaa na kuendeleza mfumo wa uimarishaji utendaji kazi kwa watumishi wa Kamisheni.
 • Kuandaa na kufanya mapitio ya Mpango Mkakati (Strategic Plan) wa Kamisheni.
 • Kuandaa Makadirio na Makisio ya matumizi (Bajeti) ya Kamisheni.
 • Kuandaa na kusimamia Mkataba wa Huduma kwa Umma (Clients Service Charter) wa Kamisheni.
 • Kutunza kumbukumbu mbali mbali zinazohusiana na utumishi wa umma.
 • Kuandaa na kuendeleza Mfumo wa Ufuatiliaji na Tathmini (Monitoring & Evaluation Frame Work) ya Utendaji Kazi wa Kamisheni.
 • Kuandaa na Kusimamia masuala ya kiutumishi ikiwemo mahitaji na maslahi ya wafanyakazi, Miundo na mambo mengineyo ya kiutumishi yanayohusu Kamisheni.
 • Kuandaa, kuweka na kutunza takwimu za kazi za Kamisheni.
 • Kuratibu tafiti mbali mbali za masuala ya Utumishi wa Umma na kutafiti masuala ya Utumishi wa Umma ndani ya Kamisheni.
 • Kuhifadhi na kutunza kumbukumbu za Kamisheni.
 • Kusimamia masuala mtambuka.
 • Kuratibu na kukuza mahusiano na Taasisi mbali mbali.
 • Kuratibu vikao vya Kamisheni.
Divisheni ya Rasilimali Watu

Divisheni hii itahusika na masuala yote ya Maendeleo na Usimamizi wa Watumishi

Divisheni ya Utawala

Divisheni hii itahusika na masuala ya Uendeshaji na Usimamizi wa Shughuli za kila siku za Taasisi.

Divisheni ya Mipango na Takwimu.

Divisheni hii itahusika na shughuli za uandaaji na ufatiliaji wa mipango ya taasisi na kushughulikia masuala ya bajeti ya Kamisheni.

Mariam R. Mbarouk

Mkurugenzi- Idara ya Rasilimali Watu, Utawala na Mipango

Subscribe to our newsletter

Sign up to receive latest news, updates, promotions, and special offers delivered directly to your inbox.
No, thanks