Kamisheni ya Utumishi wa Umma - ZanzibarKamisheni ya Utumishi wa Umma - ZanzibarKamisheni ya Utumishi wa Umma - Zanzibar
+255 (24) 2230034
kamisheni.utumishi@zpsc.go.tz
Zanzibar, Tanzania
Kamisheni ya Utumishi wa Umma - ZanzibarKamisheni ya Utumishi wa Umma - ZanzibarKamisheni ya Utumishi wa Umma - Zanzibar

Idara ya Ukaguzi, Rufaa na Malalamiko

  • Home
  • Idara ya Ukaguzi, Rufaa na Malalamiko
Maelezo
IDARA YA UKAGUZI, RUFAA NA MALALAMIKO

Idara hii itahusika na kufanya ukaguzi, uchunguzi, upelelezi, ufuatiliaji na tathmini ya utendaji wa masuala ya kiutumishi katika Taasisi za Umma. Aidha Idara itashughulikia rufaa na malalamiko yanayowasilishwa Kamisheni. Kamisheni pia itafanya tafiti mbali mbali katika masuala ya Utumishi wa Umma.

Idara hii itaundwa na divisheni tatu (3) ambazo ni divisheni ya Ukaguzi, Divisheni ya Rufaa na Malalamiko na Divisheni ya Utafiti. Idara hii itaongozwa na Mkurugenzi.

Majukumu

  • Kufanya ziara za ukaguzi, uchunguzi na upelelezi katika taasisi za umma kwenye masuala yanayohusiana na Utumishi wa Umma.
  • Kupendekeza njia bora na mifumo ya uendelezaji na usimamizi wa Utumishi wa Umma.
  • Kuandaa Mfumo wa ufuatiliaji na tathmini unaohusu utumishi wa umma.
  • Kupokea na kusikiliza malalamiko kutoka kwa watumishi na wadau mbali mbali wa utumishi wa umma.
  • Kupokea na kushughulikia rufaa zilizowasilishwa Kamisheni.
  • Kutayarisha ripoti ya utekelezaji wa kazi za idara.
  • Kufanya utafiti unaohusiana na kazi za idara.
  • Kutayarisha ripoti ya Hali ya Utumishi wa Umma.
Divisheni ya Ukaguzi

Divisheni hii itahusika na kufanya ziara za ukaguzi, uchunguzi na upelelezi pamoja na kutoa maoni na mapendekezo kuhusiana na uzingatiaji wa Sheria, Kanuni, Miongozo na Taratibu mbali mbali katika Utumishi wa Umma.

Divisheni ya Rufaa na Malalamiko

Divisheni hii itahusika na kupokea, kusikiliza na kuchambua rufaa na malalamiko mbali mbali yatakayowasilishwa Kamisheni.

Divisheni ya Utafiti

Divisheni hii itahusika na uendeshaji wa tafiti mbali mbali zinazohusiana na kazi za Kamisheni katika usimamizi wa utumishi wa umma.

Asya M. Ali

Mkurugenzi- Idara ya Ukaguzi, Rufaa na Malalamiko

Subscribe to our newsletter

Sign up to receive latest news, updates, promotions, and special offers delivered directly to your inbox.
No, thanks