Kamisheni Yakabidhi Miundo

Katibu wa Kamisheni ya Utumishi wa Umma Nd. Kubingwa Mashaka Simba amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imepiga hatua kubwa kuleta mabadiliko katika Utumishi wa Umma.

Akikabidhi Miundo ya Utumishi kwa Baraza la Ushindani halali wa Biashara na Shirika la Mawasiliano Zanzibar huko Mwanakwerekwe Nd. Kubingwa amesema uimarishaji wa maslahi ya Watumishi wa Umma hivi sasa yanategemea Miundo hiyo jambo ambalo hapo kabla halikufanyika.

Alisema Serikali imechukua jukumu kubwa kuidhinisha miundo hiyo ili kusimamia Rasilimali watu kwenye Utmishi wa Umma.

Hivyo Katibu Kubingwa amezihimiza taasisi za Umma kuteitekeleza kwa vitendo miundo yao ya Utumishi ili kuimarisha utendaji na utoaji wa huduma.

Alisema kukabidhiwa kwa miundo hiyo ni Hatua nyengine muhimu kwani inazisaidia Taasisi kungeza nyenzo katika utumishi na majukumu yao ya kila siku.

Amesema Kamisheni ya Utumishi wa Umma ipo tayari kushirikiana na taasisi hizo katika masuala ya kitaalamu hasa pale panapotokea changamoto katika utekelezajii wa Miundo ya Utumishi

Nae Mrajis wa Baraza la ushindani halali wa Biashara Nd. Fatma Gharib Haji ameahidi kusimamia utekelezaji wa Miundo hiyo ya Utumishi kwani ndio inatayochochea ari na nguvu  ya utendaji.

Nd. Fatma ameishukuru Kamisheni ya Utumishi wa Umma kwa kufanikisha jukumu hilo na kuongeza kuwa kazi iliyobaki ni kwenda kutoa elimu kwa watumishi wake kuhusu miundo hiyo.