Tamko la Katibu
Suala la kuimarisha Utumishi wa Umma ni moja ya vipaumbele vya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ). Serikali hii inatambua na kuamini kwamba, kuwa na Utumishi wa Umma wenye kutekeleza majukumu kwa ufanisi ni moja ya nyenzo muhimu katika kutoa huduma bora kwa wananchi na kuleta maendeleo endelevu katika jamii. Serikali katika kutekeleza kipaumbele hicho, imekuwa na historia ya kufanya mageuzi katika Utumishi wa Umma tokea kuasisiwa kwa Mapinduzi Matukufu ya mwaka 1964 na kuendelea na mkakati huo kwa kutayarishwa Sera ya Utumishi wa Umma ya mwaka 2010, Sheria ya Utumishi wa Umma Na.2 ya Mwaka 2011 na Kanuni za Utumishi wa Umma za Mwaka 2014.
Aidha, mkakati wa Mageuzi ya Utumishi wa Umma ulitayarishwa mwaka 2010 na kufanyiwa mapitio ya utekelezaji wake mwaka 2012. Mkakati huo umeelezea maeneo ya utekelezaji. Miongoni mwa maeneo hayo ni kuimarisha mifumo ya utumishi, usimamizi wa rasilimali watu, usimamizi wa kumbukumbu za ofisi na utekelezaji wa mageuzi katika Serikali za Mikoa, Serikali za Wilaya na Serikali za Mitaa, Wizara, Idara, Mashirika na Taasisi za Umma Zinazojitegemea. Taasisi hizo zinaendelea kutekeleza mkakati huo kwa lengo la kufikia azma ya Serikali ya kuwa na Utumishi wa Umma ulio bora na uliotukuka.

Kubingwa M. Simba
Katibu - Kamisheni ya Utumishi wa Umma