Kamisheni ya Utumishi wa Umma - Zanzibar
Kamisheni ya Utumishi wa Umma ni chombo kilichoanzishwa kwa mujibu wa kifungu cha 116 cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, Toleo la mwaka 2010 na Kifungu Nambari 17 (1) cha Sheria ya Utumishi wa Umma Nambari 2 ya Mwaka 2012, kama ilivyorekebishwa na Sheria Nambari 5 ya Mwaka 2012. Uanzishwaji wa chombo hiki ni sehemu muhimu ya utekelezaji wa Mageuzi ya Utumishi wa Umma nchini, yanayolenga kuwa na utumishi ulio bora, wenye tija na ufanisi
Kamisheni ni chombo huru kinachojitegemea chenye wajibu wa wakusimamia, kufuatilia na kushauri namna ya kuimarisha Utumishi wa Umma Zanzibar. Kamisheni imeanza kazi rasmi mwezi Septemba, 2011 ambayo imeundwa na Mwenyekiti, Wajumbe sita (6) na Katibu, ambao wote huteuliwa na kuapishwa na Mheshimiwa Rais wa Zanzibar.
Kazi kubwa ya Kamisheni ya Utumishi wa Umma ni kufuatilia na kusimamia uendeshaji wa shughuli za Rasilimali Watu katika Taasisi za Umma na kuhakikisha kuwa Utumishi wa Umma unaendeshwa kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu.
Dira
Dhamira

Kubingwa Mashaka Simba
Katibu - Kamisheni ya Utumishiwa Umma Zanzibar
Idara za Kamisheni
Waliosema Viongozi wetu
Ni maneno ya hekima yenye lengo la kuinua na kuongeza ufanisi kwa Watumishi wa Umma nchini

Dr Shein
