Watumishi wa Kamisheni ya Utumishi wa Umma wamepatiwa mafunzo maalumu juu ya mpango mkakati wa miaka mitano, wenye lengo la kuengeza uwajibikaji, ufanisi na ushirikiano katika utekelezaji wa Majukumu ya Taasisi hiyo.
Mafunzo hayo yatawajengea watumishi uwelewa wa kina kuhusu malengo , Muongozo na Mikakati ya Kamisheni katika Kipindi cha Miaka mitano ijayo ili kuhakikisha kila mmoja anachangia Ipasavyo katika kufikia matokeo tarajiwa.
Akiwasilisha mpango mkakati wa Taasisi hiyo Afisa huko
Ofisini kwake Mwanakwerekwe Afisa Takwimu wa Kamisheni ya Utumishi wa Umma Nd. Othman Haji Othman alisema kuwa na mpango mkakati madhubuti wa Taasisi ni nyenzo muhimu inayo saidia kupanga matumizi kwa vipaumbele vya Kamisheni ikiwemo kusimamia rasilimali kwa Ufanisi na kupima mafanikio ya Taasisi kwa kipindi husika.
Alisema mpango huo makakati uliojumuisha majukumu na Muundo wa Kamisheni utasaidia kuongeza uwajibika na uwajibishaji pamoja na kuimarisha mawasiliano katika Taasisi.
Ndg. Othman alisema kuna umuhimu wa Kamisheni Kutumia mpango Mkakati katika kuwezesha kutathmini maendeleo yake kila baada ya muda ulioekwa.
Alizitja faida za mpango huo mkakati ni pamoja na kuweka misingi imara ya uwazi,kuongeza uwajibikaji na uwajibishaji na kuimarisha mawasiliano katika Taasisi.
Aidha alisema Kamisheni itaendelea kutoa mafunzo endelevu kwa watumishi wake, ili kujenga utumishi bora na utendaji unaoenda sambamba na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuboresha mifumo ya Utumishi wa Umma .
Nae Mkurugenzi Utawala Rasilimali watu na Mipango Nd. Maryam Rished Mbarouk alisema kila Mtumishi ana wajibu wa kuutekeleza mpango huo mkakati wa Kamisheni katika kufikia malengo ya Taasisi.
Mkurugenzi Maryam alitoa wito kwa Watumishi kuendeleza ushirikiano , umoja na mawasiliano mazuri katika utekelezaji wa Majukumu yao kwani utekelezaji mzuri wa Mpango mkakati husaidia Kamisheni kuwa na Mashirikiano mazuri baina ya Uongozi na watumishi
Kwa upande wake Mkurugenzi Idara ya Ukaguzi Rufaa na Malalamiko Nd Asya Mussa Ali kila mmoja anapaswa kuuelewa mpango huo na kila kilichomo ndani yake kwani utekelezaji wake unakwenda sambamba na mipango mikuu ya kitaifa,dira na ilani
Akifunga mafunzo hayo Katibu wa Kamisheni ya Utumishi wa Umma Nd. Kubingwa Mashaka Simba aliwataka Wafanyakazi hao kuandaa vikao vya mara kwa mara vya kujadiliana na kujifunza mambo mbali mbali ya Taasisi kwani itasaidia kuondoa changmoto zilizopo.

