Wakala wa Barabara Zanzibar umetakiwa kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Muundo wa Taasisi yao ulioidhinishwa na Serikali.
Akitoa mafunzo ya Kujenga uelewa juu ya utekelezaji wa muundo huo huko Saateni Mkuu wa Divisheni ya Miundo ya Mawizarra Wakala Tendaji na Mashirika ya Umma kutoka Kamisheni ya Utumishi wa Umma Nd. Muhsin Ame Ali amesema kusimamiwa kwa muundo huo kutasaidia kuondoa vikwazo vya utendaji na kutoa huduma bora kwa jamii.
Amefahamisha kuwa ikila mtumishi na kiongozi wa Ofisi hiyo anatakiwa kuelewa majukumu yake na Taasisi yake ili kuepuka muingiliano katika utekelezaji wa majukumu yao.
Naye Afisa Uchambuzi Miundo kutoka Kamisheni ya Utumishi wa Umma Nd. Ame Shaame Ali amesema faida kubwa ya kuwa na Muundo wa Taasisi ni kuwa na mfumo mzuri wa uwajibikaji kwa Watumishi.
Mapema akifungua mafunzo hayo Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Barabara Zanzibar Nd. Cosmas Masolwa amesema mafunzo hayo ni muhimu kwani Wafanyakazi wengi hawana uelewa jkuhusu muundo huo.