Matumizi ya TEHAMA katika Ofisi

Wafanyakazi wa kamisheni ya Utumishi wa Umma wametakiwa kutumia mifumo ya kidigital ili kuimarisha utendaji katika utekelezaji wa majukumu yao.

Hayo yameelezwa na Mkuu wa kitengo cha TEHAMA Kutoka kamisheni hiyo Bw Machano Omar Machano wakati akitoa mafunzo kwa watumishi wa Kamisheni ya Utumishi wa Umma juu ya kuielewa mifumo ya serikali, mafunzo hayo yaliyofanyika tarehe 16 April, 2024, katika makao makuu ya ofisi hiyo iliyopo Mwanakwerekwe.

Amesema dunia hivi sasa ipo katika mabadiliko ya Teknologia hivyo, watumishi wanatakiwa kwenda sambamba na mabadiliko hayo ambyo ni muhimu katika taasisi zao.

Amesema mafunzo hayo yametolewa ili kuondoa changamoto na matatizo waliyokuwa wakiyapata hapo kabla katika matumizi ya mifumo hiyo.

Amefahamisha kuwa serikali imeingia katika mifumo ya kidigital ikiwemo eOffice, ZGMS, ZanVibal na ZanAjira, eproz n’k ili kuongeza ufanisi na kupunguza gharama hivyo kinachotakiwa ni kuanza utekelezaji.

Aidha amewasisitiza wafanyakazi hao Kuwa na natumizi sahihi ya Kompyuta katika sehemu za kazi ili kuepuka uharibifu wa mara kwa mara wa kifaa hicho.

Kwa upande wake Katibu wa Kamisheni ya Utumishi wa Umma Bw Kubingwa Mashaka Simba amewaomba watendaji hao kujiandaa kutumia mifumo hiyo kwani itafika wakati mifumo ya kawaida (Manually) haitotumika maofisini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *