Serikali ya mapinduzi ya zanzibar imekuwa ikifanya marekebisho ya mùundo kwa taasisi zake ili kuondoa changamoto za kiutendaji kwa Taasisi hiyo.
Akikabidhi muundo mpya wa utumishi kwa kampuni ya Uunganishaji na usambazaji maudhui zanzibarZMUX huko ofisini kwake Mwanakwere katibu wa Kamisheni wa utumishi wa Umma ndugu kubingwa mashaka Simba.
Amesema muuundo huo umejadiliwa na kufanyiwa marekebisho na kamidheni hiyo na hatimaye kuidhinishwa na Serikali kuu ili uendane na wakati na kukidhi mahitaji ya sasa Katika kuimarisha utumishi wa umma
Akipokea muuundo huo mkurugenzi pamoja na mwemyekiti wa ZMUX bwana na Hiji Dadi Shajak na ndugu Hasan Simba Hasan wamesema muundo huo mpya unaenda kuleta mabadiliko kwa vile watasimamia kuondoa changamoto zilizo kuwa zikiwakabili.
Mapema mkurugenzi wa idara ya Miongozo na uchambuzi wa miundo kutoka Kamisheni ya Utumishi wa Umma bwana Gharib Khamis Mustafa ameishukuru Kampuni ya ZMUX kwa ushirikiano wake katika muda wote wa kufanya kazi hatua iliyosadia kufanikisha vyema jukumu hilo.