Ziara ya Ukaguzi Manispaa Magharib A

Afisi ya Rais Kamisheni ya utumishi wa umma imewataka watendaji wa Baraza la Manispaa Magharibi A. kuzingatia mkataba wa Huduma kwa umma ili wananchi wapate huduma bora na kwa ufanisi.

Akizungumza na watendaji wa Baraza la Manispaa Magharib “A” katika ziara ya Ukaguzi wa Rasilimali watu uliofanyika jana tarehe 11/11/2024 huko Kianga, Mkurugenzi Idara ya Utawala Rasilimali watu na Mipango kutoka Kamisheni ya Umma Bi Maryam Rished Mbarouk amesema kila mtendaji anawajibu wa kuuelewa na kufuata mkataba huo  ili kutoa huduma kwa wakati na kwa kuzingatia Sheria ya Utumishi inayomuongoza.

Amesema lengo la Serikali ni kuona Taasisi za Umma zinatoa huduma kwa wananchi bila usumbufu. Nao baadhi ya watendaji na wananchi waliofuata huduma mbali mbali katika Baraza hilo wamesema licha ya kasoro ndogo ndogo zinazijitokeza hali ya utoaji na upatikanaji wa huduma unaridhisha.

Katika Ziara hiyo pia watendaji wa Kamisheni ya Utumishi wa umma walipata nafasi ya kufanya ukaguzi katika vitengo mbali mbali ili kuangalia utekelezaji wa Sheria na Kanuni za Utumishi wa umma.